Msemaji wa ikulu ya rais Uturuki Ibrahim Kalın amepeperusha ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter akifahamisha kuwa kitabu kitakatifu cha uislamu Quran kitalindwa hadi siku ya mwisho dunia itakapotanduka.
Uturuki imejibu na kukemea vikali hatua ya baadhi ya watunzi wa vitabu na wanasiasa nchini Ufaransa waliosaini kuwa baadhi ya aya katika kitabu kitakatifu cha Quran ziondolewe wakidai kuwa zinazagaza uhalifu na chuki dhidi ya wayahudi.
Zaidi ya wanasiasa na watunzi wa vitabu zaidi ya 300 nchini Ufaransa wametia saini wakidai kuwa aya hizo ziondolewe katika Quran. Msemaji wa ikulu ya rais wa Uturuki amesema kuwa Quran ni kitabu kitakatifu na sio kitu cha kufanyia mchezo na kitalindwa hadi siku ya mwisho.
Chuki dhidi ya wayahudi ni fikri na chuki iliapandikizwa barani Ulaya na iwapo Ulaya inataraji kutatua suala hilo basi ijitathmini na kujiuliza kuhusu historia yake amesema Ibrahim Kalın.
Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevtlüt Çavuşoğlu amesema kuwa jambo hilo nchini Ufaransa linaashiria ni kiasi gani chuki dhidi ya uislamu na ubaguzi vinazidi kukita mizizi Ulaya. Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki amesema kitando hicho ni uvukwaji wa mipaka.
Historia inaonesha wazi kuwa wayahudi waliangamizwa barani Ulaya wakati ambapo Utawala wa Dola ya Uthmania na waislamu ulikuwa ukiwapa hifadhi na kuwalinda.
Uislamu hauna chuki dhidi ya wayahudi kwa kuwa ni kinyume na mafunzo , chuki dhidi ya wageni, ubaguzi wa rangi na mabaya mengine vimezidi kuongezeka barani Ulaya ikiwemo pia vyama vya kibaguzi.