Kampuni ya uzalishaji pombe ya kijerumani ya Eichbaum imeomba radhi Saudi Arabia pamoja na waislamu wote duniani.
Kampuni hiyo imeomba radhi baada ya kutoa chupa za pombe zilizokuwa na kifuniko chenye bendera ya Saudi Arabia yenye maneno ya kalimat tawhiidi كلمة التوحيد.
Kalimat tawhiid ni kusema/kuandika Laa ilaha illa Allah Muhammad Rasuul Allah لا إله إلا الله محمد رسول الله.
Kampuni hiyo inasema ilitoa chumba za namna hiyo kama kuhamasisha kampeni za michuano ya Kombe la dunia inayofanyika Russia mwezi ujao. Saudi Arabia ni moja ya washiriki katika michuano hiyo.
Kampuni hiyo imeomba radhi na kutoendelea kutoa chupa zenye mfuniko wa namna hiyo. Imesema chupa 171 ndizo zilizoingia sokoni.
kampuni hiyo yenye makao yake makuu katika mji wa Mannheim imesema haikujua maneno yaliyo kwenye bendera ya Saudi Arabia yana uhusiano na dini ya uislamu.
Kutolewa kwa chupa hizo kulilaaaniwa na waislamu duniani kote kwa kampuni hiyo kuonesha kudharau dini ya kiislamu.
kadhalika ubalozi wa Saudi Arabia mjini Berlin uliishutumu kampuni hiyo kwa kufanya jambo hilo bila ya kuwasiliana na nchi husika.