Friday, 11 May 2018

MTU MMOJA AUAWA NA WAWILI WAJERUHIWA VIBAYA MSIKITINI AFRIKA KUSINI

Watu waliokuwa na visu wamevamia mskiti unaopatikana KwaZulu Natal na kuwajeruhi watu wawili na kummalizia maisha mtu mmoja katika shambulizi lao.
Watu hao wawili waliojeruhiwa wamepelekwa hospitali wakiwa katika hali mbaya mno.
Tukio hilo limeripotiwa kutokea Alhamisi kama ilivyofahamishwa na Polisi ambayo imefahamisha kuwa watu hao  waliokuwa  wamevamia kwa visu walijaribu  kuwachinja watu watatu.
Uchunguzi wa polisi unaendelea na bado wahusika wa shambulio hilo hawajatiwa nguvuni wala kubainika chanzo ni nini.