Tuesday, 20 February 2018

MKE WA SHEIKH ABOUD ROGO AHUKUMIWA MIAKA 1O

Mahakama imemuhukumu miaka 10 hatia Haniya Said Saggar kuratibu shambulio la bomu la petroli lililotekelezwa dhidi ya kituo cha polisi jijini Mombasa miaka miwili iliyopita. 
Haniya Said
Haniya ni mjane wake Sheikh Aboud Rogo, ambaye aliaminika kuandaa shughuli za kundi la wanamgambo wa Al Shabaab nchini Kenya.

Kwenye hukumu yake, hakimu alisema kulikuwa na ushahidi wa kutosha kwamba Haniya aliwasiliana na mmoja wa wanawake watatu waliolitekeleza shambulio hilo.

Mwanamke huyo, Tasnim Yakub, alikuwa amesilimu kutoka Ukristo miezi mitatu kabla ya shambulio, ikiwa ndio muda pia ambao alipata kujuana na Haniya.

Mahakama imefahamishwa pia kwamba wawili hao waliendelea kuwasiliana hadi muda mfupi kabla ya shambulio hilo.

Inadhaniwa pia kwamba Tasnim aliwavutia wanawake wawili aliojiunga nao kukiteketeza moto kituo cha polisi na hata kujaribu kumdunga kisu askari. Wote watatu walipigwa risasi na kuuawa.

Ripoti ya ushahidi uliotokana na uchunguzi umebaini kwamba kipakatilishi cha Tasnim kilikuwa na fasihi zenye itikadi kali baadi ambazo zilichapishwa na kiongozi wa kidini mweye misimamo mikali Aboud Rogo - marehemu mumewe mshtakiwa.

Rogo mwenyewe aliuawa kwa kupigwa risasi mara kumi na sita na watu wasiojulikana mnamo mwaka 2012 , tukio ambalo lilizua maandamano na tafrani jijini Mombasa.