Naib Mudir wa Mahdi(chuo kikuu) Shamsul Maarif ya jijini Tanga Sheikh Rashid bakar Al Burhani amefariki leo jioni katika Hospitali moja binafsi mkoani humo.
Naib Mudir alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa takribani wiki moja na alikuwa amelazwa hopitalini.
Taarifa za kufariki kwake zimepatikana muda wa saa 12:45 jioni.
Sheikh Rashid Bakar Al Burhani alitawazwa rasmi kuwa Naibu Mudir tarehe 16 April mwaka 2016 katika siku iliyofanyika Khitma ya Al marhumu Sheikh Muhammad Bakar Al- burhan.
Kabla ya kuwa Naib Mudir alikuwa akifahamika kama Mushrif chuoni hapo na ndugu na Marehemu Sheikh Muhamad bakar aliyekuwa Mudir wa Shamsul maarif.
Taarifa zaidi za mazishi yake tutawafahamisha pale taarifa rasmi itakapotolewa.
Endelea kufatilia Blogu ya Ahbaabur rasuul kwa taarifa zaidi.