Bakwata imekanusha kwamba hakuna njama zozote za kumuondoa mufti madarakani na hakuna ubadhirifu
wowote anaotuhumiwa Mufti.
Aidha taarifa hiyo imesema katika kipindi cha Mufti Abubakar Zubeir baraza limeimarika na kufanya mambo yake kwa mujibu wa katiba yake kuliko kipindi kipindi chochote.
Kanusho hilo limekuja kufuatia madai yaliyotolewa kupitia mitandao ya kijamii kwamba Bakwata kuna mgogoro unaowahusisha baadhi ya wajumbe wa baraza la ulamaa Taifa, Wajumbe wa Halmashauri Kuu na Masheikh
wa Mikoa ya Dar es salaam na Tabora kutaka kumuondoa Mufti madarakani kwa tuhuma za ubadhirifu
wa mali na kushindwa kuliongoza Baraza.
Wakati huo huo, Baraza hilo pia limekiri kukabiliwa na ukata kiasi cha kushindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi wake huku likidaiwa shilingi milioni 176 ambazo ni pamoja na malimbikizo ya mishahara ya wafanyakazi wake tangu mwaka 2016.