Msimamizi wa misikiti miwili mitakatifu (Madina na Makkah) amemtaka imamu wa msikiti wa Mtumeﷺ wa madina kurudi nyuma na kuanza kutumia mihrabu ya zamani iliyokuwepo katika msikiti huo.
Agizo hilo lilitolewa kupitia tovuti yake na tayari hatua zimeanzwa kufuatwa.
Katika swala ya ijumaa ya wiki iliyopita Imamu wa msikiti wa madina alisalisha swala hiyo kwa kuongoza akisimama katika miharabu hiyo ya zamani.
Hatua hii imekuja ili kurahisisha na kuondoa usumbufu kwa waumini wanaotaka kumsalimu Mtumeﷺ pamoja na maswahaba zake wawili Saydna Omarرضي الله عنه na Saydna Abubakarرضي الله عنه ambapo makaburi yao yapo ndani ya msikiti huo kwa mbele.
Agizo hilo litazingatia kufuatwa katika swala za Ijumaa, Eid mbili, Taraweeh, na swala za usiku.
Sheikh Ali Al-Huzaifi ndiyo alikuwa Imamu wa mwisho kuongoza swala kutoka katika Mihrabu hiyo ya Mtumeﷺ mwaka 1414H, ni sawa na miaka 25 iliyopita.
Miharabu hiyo ya zamani iliachwa kutumiwa na maimanu wa msikiti huo kutokana na kuongezwa kwa ukubwa wa msikiti huo na hivyo kutumika na waumini kusali japo rakaa mbili kupata barka ya miharbu hiyo.