Monday, 11 December 2017

SHEIKH WA AZHAR AKATAA KUKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI

Ahmed al Tayeb, sheikh wa Azhar nchini Misri amekataa kukutana na makamu wa rais wa Marekani Mike Pence akisema kuwa hawezi kukutana na watu ambao wanapotosha historia na kuwazuia watu haki zao za kimsingi.
Taarifa hiyo ilitolewa na Al Azhar kuhusu mkutano uliokuwa unatarajiwa kufanyika ifikao Disemba 20 baina ya Al Tayeb na Pence wakatika wa ziara yake katika ukanda.

Hapo awali Al Tayeb alikuwa akitarajiwa kushiriki katika mkutano uliotolewa wito na balozi wa Marekani Cairo na kufahamisha baadae kuwa Al Tayeb hatoshiriki kama ishara ya kupinga uamuzi wa Trump kuutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel