Monday, 13 November 2017

SIKUKUU YA MAULID KITAIFA KUFANYIKA MKOA LINDI MWAKA HUU

Sikukuu ya Maulid (Maulid Day) ya kuzaliwa Mtume Muhammad ﷺ kitaifa inaratajiwa kufanyika wilayani Ruangwa mkoani Lindi Mwaka huu.
Mufti Mkuu na Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar Zubaeir
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mufti Mkuu na Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar bin Zubeir alisema ni kwamba mwaka huu wamepanga yafanyike Mkoa wa Lindi.

Mufti Mkuu na Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar bin Zubeir alitoa taarifa hiyo wakati akiongea katika kipindi cha kiislamu kinachorushwa na Televisheni ya Taifa ya TBC1.

Maulid ya kitaifa yamekuwa yakifanyika kila mwaka mwezi mosi mfungo sita ambapo siku hiyo huwa ni mapumziko kwa nchi nzima kupisha sherehe za kuzaliwa mtukufu wa daraja Mtume Muhammdﷺ.

Mwaka huu Maulid Day inatazamiwa kuwa tarehe 1 Desemba.