Rayouf anasema kuwa alichoshwa kwa kushindwa kujitambua katika majukwaa ya kimataifa katika picha na alama zake za vidole: ''Kujihisi kutengwa, sio uhalisia wa kweli ni kama jambo ambalo ningependa liwepo au ninaloweza lifanyike".
"Hadi pale kampuni ya Apple, ilipotoa emoji hiyo, sikujua ninavyohisi, Mimi nimekuwa mwenye furaha kubwa. Naweza hata kufa kwa furaha niliyo nayo".
Aliiambia idhaa ya BBC ya The Cultural Frontline, kuhusu namna, kupitia kazi ya uchoraji wa grafiki na ubunifu wa kisasa, kupitia mtindo wa Aphee Messer, emoji hiyo ya hijabi ikazaliwa.
Msichana huyo raia wa Saudi Arabia anayeishi Ujerumani, amebuni emoji hiyo ya ijab kwa wanawake waislamu.
Rayouf Alhumedhi, ana umri wa miaka 15, na ametuma pendekezo hilo lake hadi kwa The Unicode Consortium, shirika moja la kibinafsi lisilohitaji faida yoyote, ili emoji hiyo mpya ipigwe msasa, liundwe na kunakifishwa kabla ya kuanza kutumika.
Julai mwaka huu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Apple Tim Cook alitangaza kampuni yake imezindua Emoji ya Hijab katika siku ya kimataifa ya imoji.
Siku ya kimataifa ya emoji hufanyika kila mwaka tarehe 17 julai.
Emoji ni vibonzo vinavyotumika kuelezea ujumbe katika kurasa za WhatsApp, Facebook nk kuelezea jambo badala ya maneno.
Emoji hiyo imeanza kutumika kwa watumia wa toleo la la iOS 11.