Imeelezwa Al-Habib Umar bin Hafiz عمر بن حفيظ anakuja Tanzania kwa mwaliko wa Mufti wa Tanzania Sheikh Mkuu Abubakar Zubeir na atakaa kwa siku chache kabla ya kuondoka kuelekea nchini Kenya.
![]() |
Al-Habib Umar bin Hafiz عمر بن حفيظ |
Ujio wa Alhabib Umar ni jambo kubwa ambalo waislamu wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kwenda kumpokea katika uwanja wa ndege wa Dar es salaam.
Al-Habib Umar bin Hafiz عمر بن حفيظ ambaye ndiye Mkuu wa chuo cha Dar Al Mustafa kilichoko Tarim, Yemen, inaaminika mbali na Usomi wa dini aliokuwa nao pia ni mchamungu wa kikweli.