Rais wa uturuki Recep Tayyıp Erdoğan atazungumzia kuhusu jamii ya Rohingya inayodhulumiwa Myanmar katika mkutano wa Umoja wa Mataifa unaotarajiwa kufanyika ifikapo September 19.
Akiwa mjini Istanbul, rais wa Uturuki aliwaambia raia kuwa alifanya mazungumzo na viongozi zaidi ya 20 kuhusu Myanmar na kusema kuwa katika mkutano wa Umoja wa Mataifa atazungumzia kwa kina kuhusu hali inayojiri Myanmar.
Rais Erdoğan amesikitishwa na ukimya wa jumuia ya kimataifa kuhusu mauaji ya waislamu kutoka katika jamii ya Rohingya.