Mwanazuoni wa kiislamu Daktari Sheikh Mubarak Ahmed Awes anatarajiwa kuwasili nchini kufanya ziara katika misikiti mitatu kwa kutoa mawaidha mbalimbali.
Sheikh Awes anatarajia kufanya mawaidha katika misikiti ya Dar Es Salaam.
Misikiti anayotarajiwa kuzungumza na waislamu ni Kichangani wa Magomeni siku ya jumapili septemba 10, 2017 muda wa Adhuhuri na siku hiyo hiyo pia atazungumza katika Msikiti wa Mtoro muda wa Magharibi.
Aidha siku ya jumatatu atazungumza katika Msikiti wa Dawiel uliopo Ilala muda wa Adhuhuri.
Hii si mara ya kwanza kwa Sheikh Awes kutembelea Tanzania na kuzungumza katika misikiti na waislamu.
Daktari Sheikh Awes anayetokea katika nchi ya Kenya anatajwa kama mwanazuoni kijana zaidi katika ukanda wa Afrika mashariki na msomi aliyepata sehemu ya elimu yake katika chuo kikuu cha Azhari cha Misri.