Monday, 4 September 2017

MAANDAMANO MAKUBWA KUPINGA MAUAJI YA WAISLAMU ROHINGYA YAFANYIKA INDONESIA

Raia nchini Indonesia wamemiminika mabarabarani kukemea mauaji ya jamii ya Rohyngyas Myanmar

Mauaji ya Rohingya yalianza upya mwishoni mwa Agosti na kusababisha maelfu ya watu kuhama makaazi yao na kutafuta hifadhi katika maeneo yaliyo salama.
Maandamano makubwa yaliandaliwa mjini Jakarta kwa ajili ya kukemea mauaji na dhulma wanayotendewa waislamu jamii ya Rohingya.

Maandamano hayo yaliandaliwa Jumapili mjini Jakarta nchini Indonesia.

Katika maandamano hayo waandamanaji walikusanya kiwango cha pesa kwa ajili ya kusaidia wakimbizi wa jamii hiyo waliokimbilia nchini Bangladesh.

Taasisi kubwa za kimataifa na mashirika ya haki za binadamu yamekuwa kimya katika matukio hayo ya kuuawa kwa waislamu wa Rohingya.