Polisi wa uhamiaji wa Ubelgiji wamfukuza raia wa Denmark kwa kugoma kuvua Niqabu.
Raia huyo wa Denmrak alikuwa akitua mjini Tunis alipogoma kuvua Niqabu na matokeo yake kufukuzwa nchini Ubelgiji.
Polisi wa uhamiaji nchini Ubelgiji wamefahamisha kuwa raia huyo wa Denmark aligoma kuvua Niqabu yake jambo ambalo lilitatiza msafiri huyo kutambulika kuwa mmiliki wa hati ya usafiri.
Katibu mkuu wa uhamiaji Theo Francken alitoa taarifa hiyo katika ukurasa wa Facebook.
Mwaka 2015 Polisi wa Ubelgiji walimkamata mwanamke mmoja kutoka Saudia Arabia kwa kuvaa Niqabu na kuachiwa baada ya ubalozi wa Riyadh kuingilia kati.