Monday, 25 September 2017

MPOLAND AENDA MAKKA KWA FARASI KUJIFUNZA UISLAMU

Raia mmoja kutoka Poland atasafiri kwa kutumia farasa kuelekea Makka kujifunza uislamu.
Raia huyo kutoka Poland alietambulika kwa jina la Kristian Bergier, miezi 9 baada ya kuanza safari yake  kwa kutumia farasi amewasili Ijumaa mji wa Adiyaman kusini mwa Uturuki.
Raia huyo atajielekeza mjini Jerusalem na baadae Makka na Madina kwa lengo la kujifunza uislamu.
Raia huyo katika mahojiano aliofanya na shirika la habari la Anadolu amekariri quran  na anajielekeza Makka kujifunza na kuelewa uislamu licha ya kuwa yeye sio muumini wa kiislamu.