Monday, 18 September 2017

JESHI LAUKOMBOA MSIKITI WA KIHISTORIA UFILIPINO

Kwa mujibu wa habari, jeshi Ufilipino limefanikiwa kuukomboa msikiti wa kihistoria wa Bato.

Msikiti wa Bato ni kati ya sehemu ambapo waislamu hutumia sana katika ibada zao za kila siku.

Msikiti huo umekombolewa baada ya kuwa umechukuliwa na wapiganaji wa Maute wenye uhusiano na kundi la kigaidi la DAESH mnamo Mei 23.

Jeshi linaamini kuwa mapigano kati ya serikali na wapiganaji wa Maute yanafikia ukingoni nchini Ufilipino.

Mpaka sasa ni sehemu nyingi zimefanikiwa kukombolewa na maafisa wa jeshi kutoka katika mikono ya kundi la kigaidi laa Maute.