Tanzania inajiandaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa nne wa uchumi wa kiislamu Afrika mwezi Machi mwaka huu.
Mkutano huo utafanyika Machi 28 na 29, 2017 jijini Dar es salaam unatarajiwa kuwa na wajumbe kutoka nchi zaidi ya 10.
Al Huda Centre of Islamic Banking and Economics (CIBE) yenye makao yake Dubai ndio walioandaa mkutano huo.
Mkutano huo unaotarajiwa kufungua milango kwa wawekezaji nje, uchumi wa kiislamu unazingatia zaidi faida ya makubaliano ya ufanyaji biashara kinyume na riba.
Ukuaji wa Uchumi wa kiisalmu kwa nchi za Afrika umekuwa ukiongezeka kila mwaka kwa asilimia kadhaa.
Tanzania imeruhusu Uchumi wa kiislamu na mpaka sasa kuna benki moja inayoendesha Uchumi wa kiislamu na baadhi ya benki kuwa Islamic Window
