Monday, 6 March 2017

QURANI KUPIGWA MARUFUKU UHOLANZI, ASEMA GEERT WIDERS

Wakati kilele cha kampeni za uchaguzi nchini Uholanzi kikifikia ukingoni, chama cha Freedom party (PVV) kimesisitiza kwamba endapo kitapata ridhaa ya kuongoza
kitapiga marufuku Qurani nchini humo.
Uchaguzi unatarajiwa kufanyika mwezi huu tarehe 15, ambapo Chama hicho kina viti 12 kati ya 150 kina imani katika uchaguzi huu kushinda viti vingi zaidi. 

Chama kitakachopata viti 70 na zaidi ndio kitakachopata mamlaka ya kuunda na kuongoza serikali katika nchi hiyo.

Kiongozi wa chama hicho Geert Wilders amesema mbele ya waandishi kwamba Qurani lazima ipigwe marufuku na ni haramu nchini humo.

Aidha, Ilani ya Uchaguzi huu ya chama hicho, ilisema itachukua hatua mbalimbali ikiwemo kufunga mipaka, 

kufunga vituo vya wakimbizi, kuzuia wahamiaji kutoka nchi za kiislamu na kuzuia wanawake wa kiislamu kuvaa Hijabu katika maeneo ya Umma.

Geert Wilders ambaye ndiye anayekiongoza chama hicho anatajwa kama mtu anayeongoza kwa chuki dhidi ya uislamu duniani. 

Geert Wilders amekuwa akienda popote duniani ili kutoa mchango wake katika harakati za kuukandamiza Uislamu.