Kampuni ya Nike inayotengeneza mavazi na bidhaa mbali mbali za michezo sasa imeanza kutengeneza hijabu kwa ajili ya wanariadha wanawake wa kiislamu .
Hijabu hizo zinazotambulika kwa jina la 'Nike Pro Hijabs' zimetengenezwa kwa kitambaa imara na cha kudumu .
Hijabu hiyo kwa sasa inatarajiwa kuwa na rangi ya nyeusi na nyeupe na zitaonyeshwa na kuingizwa sokoni majira ya kipupwe mwaka 2018.
Kampuni ya Nike ilitangaza kuwa hijabu hizo zitatengenezwa kwa wingi kulingana na utendaji bora .