Tuesday, 28 February 2017

WAISLAMU WENYE ASILI YA AFRIKA WABAGULIWA ZAIDI UJERUMANI

Shirika moja la kufatilia matukio la Umoja wa mataifa limeonya kuhusu kuongezeka kwa chuki dhidi ya waislamu waafrika nchini Ujerumani.
Ricardo Sunga, mwenyekiti mkuu wa shirika hilo la wataalamu la UN alitangaza matokeo ya utafiti uliofanywa katika mkutano jijini Berlin.

Wakati huo huo Sunga alisifia juhudi za Ujerumani katika kuhakikisha haki za binadamu zinazingatiwa nchini pia alielelezea wasiwasi wake kuhusu ongezeko la ubaguzi wa waislamu wa asili ya Afrika katika maeneo ya kazi na shule.

Mapema mwezi Februari kundi la shirika la wataalamu hao walizuru Ujerumani kufuatilia haki za binadamu zinavyozingatiwa kwa raia nchini humo.