Msikiti janja (smart mosque) unatazamiwa kuzinduliwa hivi karibuni kwa mara ya kwanza katika Umoja wa Falme za Kiarabu UAE.
Msikiti huo Janja utafunguliwa katika la Ras Al Khaimah nchini humo na watu wengi UAE wakivutiwa na kila kitu.
Msikiti huo ambao umekuwepo kwa muda mrefu katika eneo la Muairidh sasa umekarabatiwa na uko tayari kutumika kwa kuzingatia teknolojia na utafahamika ni msikiti wa ‘kijani’ kwa maana kuwa ujenzi wake umezingatia utunzwaji mazingira.
"Umeme wa vipaza sauti huwaka punde Imamu anaposimama juu ya zulia au msala katika mihrabu na huzimika wakati sala inapomalizika,” amesema Dkt. Hisham Al Refaei Al Mansuri msimamizi wa mradi huo.
Aidha anasema taa za msikiti huo zinatumia nishati ya jua na huwaka na kujizima zenyewe kwa kuzingatia wakati wa Sala na idadi ya waumini ndani ya msikiti. Dkt. Al Mansuri anaongeza kuwa, kiyoyozi (air conditioner) katika msikiti huwaka na kuzimika sambamba na kubadlisha nyuzi joto kwa kuzingatia hali ya hewa na pia wa kutegemea idadi ya watu walio ndani ya msikiti.”
Mabomba katika eneo la kutawadha hutegemea sensa maalumu ili kuzuia israfu(matumizi mabaya) ya maji.
Aidha maji yanayotumiwa kwa ajili wa wudhuu hutumiwa tena baada ya kusafishwa kwa mashine maalumu zilizopo huku maji ya mvua nayo yakikusanywa kwa akili ya kutumika kwa mimea au bustani ya msikiti.
Msikiti huo ulikarabatiwa kwa msaada wa watu na mashirika ya kutoa misaada na inatazamiwa kuwa, kwa kutumia teknolojia hizo, msikiti huo utaweza kuokoa takribani dola 2,900 kila mwaka ambazo zingetumika kulipia umeme na maji.
Mradi huo umeungwa mkono na Jumuiya ya Dar al Ber na Jumuiya ya Misaada Sharjah kwa ushirikiano na Halmashauri ya Masuala ya Kiislamu na Waqfu nchini Imarati.