Monday, 20 February 2017

WAISLAMU WAZIDI KUONGEZEKA CUBA

Waislamu wameripotiwa kuongezeka nchini Cuba na kupata eneo la kufanyia ibada.
Idadi hiyo imeonekana kuongezeka kwa haraka huku katika jiji la Havana kukionekana kufunguliwa kwa msikiti.
Taarifa zinaarifu kuwa katika siku za usoni msikiti wa kwanza utajengwa kwa ufadhili wa Saudi Arabia.
Msikiti huo utakuwa msikiti wa kwanza kujengwa katika kisiwa hicho.
Idadi hiyo wa waislamu katika kisiwa cha Cuba imefahamishwa kuongeza ambapo kwa sasa waislamu zaidi ya 3000 wanapatikana nchini humo.