Monday, 20 February 2017

QURAN IMEUZWA KWA WINGI MAONESHO YA VITABU MOROCCO

Qur'ani Tukufu ndicho kitabu kilichouzwa kwa wingi katika Maonesho ya Kimataifa ya Vitabu, Casablanca, Morocco.
Fouad Mkurugenzi wa Kituo cha Kuchapisha na Kusambaza Vitabu Morocco, ambacho kimeandaa maonesho ya mwaka huu, idadi ya nakala za Qur'ani tukufu zinazonunuliwa katika maonyesho hayo huongezeka kila mwaka.

Amesema vitabu vya hadithi na vitabu vya kujiboresha kimaisha ni kati ya vitabau ambavyo pia vilinunuliwa kwa wingi katika maonesho hayo.

Maonesho ya 23 ya Kimataifa ya Vitabu Casablanca yalianza Februari 9-19 na kuhudhuriwa na wachapishaji 700 kutoka nchi 24.

Waziri wa Utamaduni wa Morocco, Mohamed Amin Sbihi amesema maonesho hayo ni kati ya maonesho muhimu zaidi duniani. 

Aidha amesema maonesho ya mwaka huu yalikuwa na nchi 11 za kaskazini mwa Afrika ambazo zilipokea mwaliko maalumu.