Mjadala kuhusu ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Uislamu umependekezwa na kutayarishwa na naibu mwenyekiti wa chama cha Liberal Party İkra Halid.
Mjadala huo umeanzishwa kwa lengo la kuondoa utaratibu wowote unaofanikisha chuki dhidi ya Uislamu na pia aina yoyote ya ubaguzi wa rangi baina ya raia wa Canada.
Mjadala huo unatarajiwa kuungwa mkono na wanachama wote wa chama cha Liberty Party.
Aidha pia Tom Mulcair, kiongozi mkuu wa chama cha New Democratic Party alifahamisha kuwa chama chake kitaunga mkono mada hiyo .
Chama cha Conservative party kimetangaza kupinga mada hiyo mpya .
