Vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti kwamba mwana wa aliyekuwa gwiji wa ndondi nchini Marekani Muhammad Ali alizuiliwa na kuhojiwa kwa saa mbili katika uwanja wa ndege wa Florida.
Muhammad Ali Jnr aliyekuwa na mama yake Khalilah Ali mke wa kwanza wa Muhammad Ali, alizuliwa na kuwekwa katika katika chumba maalumu baada ya kuwasili kutoka Jamaica mapema mwezi huu kutokana na jina lake kuonekana la dini ya kiisalmu.
Wakili wa familia ya Muhammd Ali, Chris Mancini alinukuliwa akisema kuwa kuzuiliwa kwa Muhammad Ali Jnr kulihusishwa moja kwa moja na jaribio la rais Trump kuwapiga marufuku Waislamu kutoka mataifa saba ya Waislamu kuingia Marekani.
Muhammad Ali Jnr mwenye umri wa miaka 44 aliulizwa mara mbili kama yeye ni muislamu na wapi amelipata jina hilo na vipi ameipata Passport ya marekani.
Wakili Chris Mancini anaangalia namna ya kufunhua kesi kwa watu wa idara ya U.S. Treasury and Homeland Security ili iwe darasa kwa wengine
