Wanawake wengi wameonesha ushirikiano wa hali ya juu kwa kuazimia kuvaa hijabu kwa muda wa mwezi mzima nchini Canada.
Hii ni kama ishara ya kuonyesha ushirikiano kwa waislamu wa nchi hiyo ambapo nchini humo kumekuwa na matukio mengi ya unyanyasaji wa kidini hususani kwa waislamu.
Wanawake wa Fort McMurray wamesema watakuwa sambamba na wanawake wa kiislamu katika kuhakikisha wanapewa haki zao.
Kiongozi wa World Hijab Day Kiran Malik Khan amesema waislamu wamefurahishwa sana na mshikamano huo.
World Hijab Day ilianzishwa mwaka 2014 na wanawake wa kiisalum kuitangaza na kuonesha umuhimu wake kwa jamii isiyo ya kiislamu.

