Friday, 6 January 2017

ASKARI WA KIISLAMU WARUHUSIWA KUFUGA NDEVU NEW YORK, MAREKANI

Askari wa kiislamu katika jimbo la New York nchini marekani
wameruhusiwa kufuga ndevu kwa sababu za dini yao.
kwa mujibu wa sera mpya ya idara ya polisi New York imesema imefanya hivyo kwa lengo la ushirikishwaji wa makundi mbalimbali ya imani.

Kamishna wa Polisi James O'Neill alinukuliwa na gazeti la Times New York akisema kuwa wamefanya mabadiliko hayo ili kuruhusu kila mtu katika mji wa New York anayetaka kuomba kufanya kazi katika idara ya polisi anaweza kufanya hivyo bila ya kikwazo chochote.

Hayo yalisemwa wakati wa sherehe za mahafali kwa ajili ya kuajiri Polisi wapya. 

sheria hiyo mpya itaruhusu ndevu kukua kwa urefu sentimita 1.27 (1.27cm). Kufuga ndevu kwa mwanaume katika dini ya kiislamu ni sunna iliyohimizwa.

Wanawake wa kiislamu katika NYPD (idara ya polisi ya New York) kwa mika mingi wameruhusiwa kuvaa Hijabu.