Mgahawa mmoja wa kiislamu nchini Canada unatoa huduma ya chakula kwa watu ambao hawana uwezo wa kununua chakula.
Mmiliki wa mgahawa huo amesema kuwa huduma ya bure ya chakula kwa watu ambao hawana uwezo wa kujinunulia chakula inatolewa bila ya mtu kuulizwa swali lolote.
Mgahawa huo unapatikana katika jiji la Montreal.
Mmiliki wa mgahawa huo kwa jina la Yahya Hashemi amesema kuwa kukosa pesa ni jambo ambalo linaweza kumtokea yeyote yule katika maisha
