Baada ya miaka minne ya ndoa yake na Wissam Al Mana hatimaye Janet Jackson amejifungua salama mtoto wake wa kwanza siku ya jumanne wiki hii.
"Janet alijifungua salama na amekuwa mwenye afya nzuri", ilisema taarifa kutoka kwa msemaji msemaji wa Janet.
Msemaji huyo aliongeza kwamba familia imefurahi kumkaribisha mtoto huyo wa kiume ambaye amepewa jina la Eissa Al mana (Issa عيسى).
Issa عيسى ni jina la kiarabu alilokuwa akitumia Nabii wa mwenyezi Mungu Issa bin Mariam ambaye ametajwa katika Quran aya ya 171 katika suratil Nisaa(4).
Janet aliyejifungua akiwa na umri wa miaka 50, uvumi wa kuwa mjamzito ulienea kuanzia mwezi April mwaka jana.
Janet anaelezwa kusilimu tangu kuolewa na Tajiri wa Qatar, Wissam Al Mana na mara kwa mara amekuwa akitumia lugha za dini ya kiislamu pamoja na mavazi stara.
