Wamarekani wawili waislamu wenye asili ya kiarabu wametimuliwa kutoka kwenye ndege ya shirika la Delta jumatano wiki hii kwa kusikika wakizungumza lugha ya kiarabu.
Adam Saleh mwenye umri wa miaka 24 na rafiki yake Salim Albaher walishushwa katika ndege hiyo walipokuwa wakitoka London wakirejea mjini New York wakati walipotakiwa na rubani wa ndege ya Shirika la Delta kushuka katika ndege hiyo iliyokuwa katika Uwanja wa Heathrow mjini London.
Saleh anasema baadhi ya wasafiri walifungamana naye na kupinga hatua ya rubani huku baadhi wakishangilia alipotimuliwa kutoka katika ndege hiyo.
Salehi, ambaye amesema alikuwa akizungumza na mama yake mzazi kwa lugha ya Kiarabu, ametuma taswira ya video kuhusu tukio hilo kupitia mtandao wake wa twitter. Idadi kubwa ya watu wamebainisha ghadhabu yao katika mitandoa ya kijamii kufuatia tukio hilo la kibaguzi.
Katika video hiyo, Saleh anasikika akisema: "Nyingi ni wabaguzi, siamini ninachokiona. Wazungu sita dhidi ya watu waweli wenye ndevu. Huu ni mwaka 2016, 2016. Tizama Shirika la Delta linatutumua kwa sababu tu tunazungumza lugha tafauti."
Baada ya kuchelewa kwa masaa kadhaa, Saleh anasema hatimaye walifanikiwa kupanda ndege ya kuelekea New York lakini kwa kufanyikwa uchunguzi mkali wa kiusalama.
Amesema atachukia hatua za kisheria dhidi ya Shirika la Delta.
Katika miezi ya hivi karibuni kumeripotiwa visa kadhaa vya Waisani na Waarabu katika nchi za Magharibi wametakiwa waondoke ndani ya ndege kwa sababu ya dini yao.
