Wednesday, 21 December 2016

ATAFUTWA KWA KUVUNJA NA KUIBA PESA MSIKITINI

Polisi wa upelelezi wanamtafuta mtu aliyefunika uso wake na kuiba pesa katika Masjid Darul Quran ulioko Bayshore katika kisiwa cha Long island, kaunti ya Suffolk, jimbo la New York nchini Marekani.
Mtu huyo ambaye bado hajajulikana aliingia Msikiti mapema jumanne baada ya milango ya msikiti huo kufunguliwa saa tisa na robo za usiku kwa ajili ya maandalizi ya swala ya Alfajiri.

Kamera zilimuonesha mwizi huyo akiingia na kuvunja sanduku la kuwekea pesa wanazochanga waumini kama sadaka mnamo saa tisa na dakika arobaini .

Askari wa upelelezi wanaendelea kuchunguza kupitia picha zilizonaswa na kamera zilizokuwepo ndani ya Msikiti huo.
Masjid Darul Quran
Kiasi alichoiba hakikuwekwa wazi lakini inasemekana ni kiasi kikubwa cha pesa alichoiba.

Tukio hilo limebainika kupitia kamera za cctv zilizowekwa ndani ya Msikiti, je misikiti yetu kuna haja nayo kuweka camera za namna hiyo ili kubaini matukio kama hayo?

Nini maoni yako kuhusiana na taarifa hiyo? usisite kutuandkia maoni yako.