Rais Barack Obama amefutilia mbali mpango ulionzishwa kuwasajili waislamu na wahamiaji kutoka nchi za kiislamu ulioanzishwa baada ya shambulizi la Septemba 11.
Msemaji wa wizara ya usalama wa ndani Neema Hakim alisema kuwa programu ya kufuatilia uingiaji na utokaji wa kitaifa maarufu kama NSEERS umekuwa ukitumiwa kuanzia mwaka 2011 umesimamishwa .
Waziri wa sheria katika jimbo la New York Eric Schneiderman alisema kuwa programu hyo pia ilisaidia kufuatilia shughuli ya uingiaji na utokaji.
Hata hivyo Donald Trump ambaye ataapishwa Januari 20 ataanza kazi kama rais na inakisiwa mpango huo huenda ukarudishwa kwani anaunga mkono kusajiliwa kwa waislamu na wahamiaji kutoka nchi za kiislamu .
