Thursday, 15 December 2016

UTAFITI: IDADI YA WAISLAMU YAONGEZEKA NCHI ZA ULAYA

Katika kila watu 100 katika nchi yako, unadhani waislamu ni wangapi? 

Swali hilo liliulizwa na kampuni maarufu ya utafiti ya nchini Uingereza ya Ipsos MORI kutaka kujua idadi ya waislamu katika nchi kadhaa duniani.
Utafiti huo uliofanywa kwa nchi 40, unaonesha kuwa na ongezeko kubwa la waislamu katika nchi za ulaya ambapo awali idadi yao ilikuwa ndogo.

Nchi ya Ufaransa waliohojiwa wanasema kuna waislamu 31 katika kila watu 100 katika nchi yao, lakini idadi sahihi inayotambulika ni kwamba waislamu ni asilimia 7.5 ya wananchi wote nchini humo.

Nchini Ujerumani ambapo Waziri mkuu wake Angela Merkel hivi karibuni alipiga marufuku Burqa, watu waliohojiwa wanasema idadi ya waislamu ni asilimia 16. 

Marekani inakadiriwa kuna waislamu 16 katika kila watu 100, lakini idadi halisi inasema waislamu ni asilimia 1 tu ya wamarekani wote.

Aidha nchi za Korea Kusini na Japani kumeonesha idadi ndogo zaidi ya waislamu. Katika utafiti huo imeonesha kuna waislamu asilimia 6 kwa nchi hizo.

Utafiti huo unaonesha mwaka 2020 uislamu utakuwa moja ya dini kubwa katika nchi za Ulaya na Amerika.

Je una maoni gani kuhusiana na utafiti huo? usisite kutuandikia maoni yako.