Sunday, 18 December 2016

RAIS BUHARI ATAJWA ORODHA YA WAISLAMU 500 WENYE USHAWISHI ZAIDI DUNIANI

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari jina lake limekuwa kati ya viongozi wa juu 50 wenye ushawishi mkubwa zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu.
Rais Buhari
Kwa mujibu wa orodha mpya ya mwaka 2017 ya waislamu 500 wenye ushawishi zaidi duniani, Rais Buhari amekuwa nafasi ya 17. Mwaka uliopita alikuwa nafasi ya 20.

Orodha hiyo hutolewa na Taasisi isyo ya kiserikali ya Royal Islamic Strategic Studies Center iliyo na maskani yake katika mji wa Amman, nchini Jordan.

Orodha hiyo hukusanya vingozi wa dini, wasomi wakubwa wa kiislamu, wafanyabiashara, wasanii, wanamichezo pamoja na wasomaji wa Quran.

Royal Islamic Strategic Studies Center imekuwa ikifanya mchakato wa kutoa orodha ya waislamu maarufu zaidi duniani tangu mwaka 2009.
Dr Sheikh 
Utaratibu wao ni kuwapa nafasi waislamu popote duniani kupendekeza jina au majina ya waislamu katika ngazi zote kisha huwekwa orodha itakayopigiwa kura na baadae hupangwa kwa nafasi kulingana na kura walizopata.

Katika orodha hiyo ya mwaka 2017 nafasi ya kwanza imechukuliwa na Sheikh mkuu wa Chuo kikuu cha Azhar nchini Misri Dr Sheikh Ahmad Muhammad Al-Tayyeb, Nafasi ya pili imekwenda kwa Mfalme wa Jordna Abdullah II ibn Al-hussein na nafasi ya tatu imechukuliwa na Mfalme wa Saudi Arabia Salamn bin Abdul-Azizi Al-Saud.

Kiongozi wa Iran Ayatollah Hajj Sayyid Ali Khamenei(4), Mfalme Mohammed VI wa Morocco(5), Sheikh Muhammad Taqi Usmani(6) na Ayatollah Sayyid Ali Hussein Sistani wa najaf Iraq(7). 

Wengine ni Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan(8), Sheikh Abdullah Bin Bayyah rais wa jukwaa la kuhimiza amani katika jamii za kiislamu(9) na Hajji Mohammed Abdul-wahhab amiri wa Tabligh Jammat ya Pakistan(10).