![]() |
| Sheikh Miladu Kaluuma akizungumza na waumini jana |
Aidha alisema wanamshikilia mtuhumiwa mmoja kuhusika na mauaji hayo. Alisema uchunguzi bado uanaendelea.
Msikiti wa Nakasero wenye vuguvugu la Tabliq ulivamiwa na Polisi siku ya jumanne katika kile kinachodaiwa kufanya upekuzi.
Hata hivyo taarifa hizo za Polisi zimekanushwa vikali na kiongozi wa Msikiti huo Sheikh Miladu Kaluuma kwamba si kweli na taarifa hizo zinakusudia kuchafua wana Tabliq kwamba ni wauaji.
Alisema polisi wanatumia vyombo vya habari dhidi yao. "Tunataka kumwambia kila mtu ambaye aliambiwa kwamba
polisi walikuta silaha za mauaji hapa, basi watafute hadithi nyingine kwa sababu hiyo haitafanya kazi", alisema Sheikh Kaluuma kuwaambia waumini wakati wa swala ya Adhuhuri jana katika msikiti wa Nakasero.
Pia amewataka Polisi kurudisha pesa walizochukua wakati wa uvamizi huo uliofanyika jumanne usiku, pamoja na Kompyuta, Kamera ya video, nyaraka na faili mbalimbali za msikiti huo.
Ausi bua Ogwang kiongozi wa Tabliq amesikitishwa na kitendo cha polisi kuvamia usiku na kukamata waumini
takribani 18.
Alisema ikiwa polisi wanawashuku kwa ubaya wowote waende tu mchana na wakague kwa njia iliyo ya kistaarabu wao hawana tatizo lolote.
Msako huo ni upelelezi la wimbi la kuuawa Masheikh nchini Uganda.
