Waislamu wote wa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam wanaalikwa katika sherehe za maulid ya mtume Muhammadﷺ yatakayofanyika katika Markazi Iliyopo Majohe Rada/Gongo La Mboto Siku ya Jumanne kesho tarehe 6/12/2016.
Shughuli kihistoria iliasisiwa na Al marhoum Ustaadh Muhammad Bin Shareef Saydil Biydh, inatarajiwa kuanza saa nne asubuhi na kuisha saa saba mchana.
Miongoni mwa Wageni wanaotarajiwa kuhudhuria ni Sayyid A'rif , Shabiihu Sayyid Abdallah Na Shareef Ja'afar Swaadiq ambao ni watoto wa Almarhoum Ustaadh Muhammad Bin Shareef Saydil Biydh.
Sherehe hizo zinasimamiwa na kuongozwa na Imamu msaidizi wa Msikiti wa kitumbini Ustaadh Jumaa Sha'abaan aliyewahi kuwa Imamu mkuu wa Msikiti wa Idrisa.
