Televisheni moja ya israel imedukuliwa na watu wasiojulikana
kwa kukata matangazo yake na kuweka picha na sauti ya Adhana.
Televisheni hiyo inayojulikana kama Channel 2 hurusha matangazo yake kwa njia ya Setelaiti.
Tukio hilo lilitokea jioni ya siku ya Jumanne wakati wa kuingia swala ya magharibi ndipo ghafla matangazo yaliyokuwa yakiendelea kukatika na kuingia picha ya msikiti iliyokuwa ikiambatana na sauti ya Adhana.
Licha ya kuwekwa Adhana pia kulipita maandishi yaliyokuwa katika lugha ya kiebrania yaliyosema "Adhabu kutoka kwa Mungu" na "Moto uliochoma mioyo".
Televisheni ya channel 2 huangaliwa zaidi na watu wa kaskazini mwa Israel, bado haijajulikana ni nani aliyehusika
katika udukuzi wa matangazo hayo.
Israel inataka kupitisha sheria ya kuzuia kutumia vipaza sauti kwa ajili ya Adhana jambo ambalo limepelekea malalamiko kutoka kwa waislamu wa huko.