Kundi la watu wasiojulikana limeripotiwa kuushambulia msikiti wa Rinkeby kwa mawe katika mji mkuu wa Stockholm nchini Sweden.
Mashambulizi hayo yamesababisha uharibifu mkubwa wa vioo vya msikiti huo pamoja na ofisi ya shirika la usimamizi.
Hata hivyo hakuna majeruhi wowote walioripotiwa kwenye mashambulizi hayo.
Idara ya polisi ya Sweden imetangaza kuanzisha uchunguzi ili kubainisha wahusika wa mashambulizi hayo.
