Wednesday, 16 November 2016

MAONESHO YA MAVAZI YA KIKE YA KIISLAMU KUFANYIKA JAPAN NOVEMBA 23-24

Maonesho ya kwanza ya mavazi ya kike ya Kiislamu yamepangwa kufanyika tarehe 22-23 Novemba katika mji wa Tokyo, nchini Japan.

Kwa mujibu wa gazeti la Japan Times, maonesho hayo yatakuwa maalumu kwa ajili ya mavazi ya Kiislamu ya Hijabu yanayotumiwa na wanawake Waislamu.
Waandalizi wa maonesho hayo wanasema sababu kuu ya kuyaandaa ni ongezeko la watalii Waislamu nchini Japan. 

Mbali na kujitahidi kuimarisha uhusiano wa Japan na nchi za Kiislamu, maonesho hayo pia yanalenga kuondoa dhana potofu iliyopO kuhusu mavazi ya Kiislamu.

Kwa ujumla kutakuwa na maonesho manne pamoja na warsha ya miundo ya vazi la Hijabu katika siku hizo mbili.

Maonesho hayo ya mavazi ya kike ya Kiislamu yatafanyika mjini Tokyo sambamba na maonesho ya vyakula, bidhaa na huduma Halal.