Saturday, 5 November 2016

WATU 15 WAKAMATWA KWA KUFANYA MAANDAMANO YA KUPINGA UJENZI WA MSIKITI UGIRIKI

Watu wapatao 15 wamekamatwa na polisi kwa kosa la kufanya maandamano na kukalia kwa nguvu eneo linalotarajiwa kujengwa Msikiti katika jiji la Athens nchini Ugiriki.
Kundi hilo la watu wenye msimamo linapinga ujenzi wa msikiti katika mji wa Athens kwa chuki za dini bila ya kuwa na hoja za msingi.

Kikosi cha Polisi kililazimika kuingilia kati na kuwasambaratisha waandamanji hao ambapo watu 15 walikamatwa na kuwekwa rumande.

Ujenzi wa msikiti huo umecheleweshwa kutokana na sababu za kisheria ambazo zinatarajiwa kumalizika hivi karibuni.

Hatua kubwa ilipigwa baada ya bunge la Ugiriki kupitisha mswada wa sheria unaotoa matumaini ya kuanza ujenzi wa msikiti huo.

Waziri Ömer Çelik katika ziara yake nchini Ugiriki alifahamisha kuwa hakuna tatizo kuwepo na makanisa, miskiti na masinagogi na wala hakuna uhatari wowote iwapo msikiti utajengwa Athens licha ya baadhi ya watu kuonesha ubaguzi na chuki dhidi ya waislamu.

Athens ndio mji mkuu pekee katika nchi za ulaya usiokuwa na msikiti.