Mkurugenzi katika idara ya masuala ya dini nchini Uturuki amesema kuwa mpango wa kupiga marufuku adhana katika jiji la Jerusalem ni jambo ambalo halitokubalika.
Kiongozi wa idara ya masuala ya dini nchini Uturuki Mehmet Görmet ametoa msimamo wake kufuatia mswada wa sheria nchini Israel ambao unataraji kupiga marufuku adhana mji wa Jerusalem.
Mswada huo wa sheria unalenga kupiga marufuku adhana katika vipaza sauti katika misikiti mjini Jerusalem na katika vitongoji vinavyopatikana katika maeneo tofauti.
Hayo Mehmet Görmez aliyafahamisha kwa waandishi wa habari baada ya kufanya mkutano na mkurugenzi wa masuala ya dini wa Qatar mjini Doha.
