Wananchi wa Palestina walijumuika na Hamas kwenye maandamano ya kupinga kanuni inayopiga marufuku adhana katika ukanda wa Gaza iliyowekwa na bunge la utawala wa Knesset nchini Israel.
Maandamano hayo yaliyoandaliwa na kundi la Hamas katika eneo la Jibaliya kaskazini mwa Gaza, yalianza katika msikiti wa Hulefa-i Rashidin.
Waandamanaji walitoa kauli mbiu za kupinga vikali kanuni hiyo iliyolenga kupiga marufuku matumizi ya vipaza sauti kwa ajili ya adhana.
Mbunge mmoja wa Hamas Yusuf el-Sherafi alitoa maelezo na kusema kwamba kanuni hiyo ni ya ubaguzi iliyowekwa kwa ajili ya kuumiza hisia za Waislamu.
Yusuf aliongezea kusema kwamba kanuni hiyo haiwezi kukubalika wala kupitishwa bungeni huku akisisitiza kuwa sauti za adhana zitaendelea kusikika kama kawaida.
Yusuf pia alitoa wito kwa Waislamu wote wa maeneo ya Jerusalem na Mukaddas kujitokeza kwa ajili ya kutetea haki yao ya imani ya kidini na kuzuia serikali ya Israel kuleta itikadi za Kiyahudi.
Maandamano hayo yalimalizika kwa sauti za adhana zilizotolewa na waandamanaji.
