Friday, 18 November 2016

MBUNGE APIGA ADHANA NDANI YA BUNGE LA ISRAEL KUPINGA MUSWADA

Mbunge wa Israel mwenye asili ya kiarabu jumatatu hii alipiga adhana ndani bunge la Israel kama ishara ya kupinga muswada uliopelekwa kwa ajili ya kupiga marufuku Sauti za Adhana katika misikiti ya Jerusalemu na katika vitongoji vinavyopatikana katika maeneo tofauti.
Ahmed Al Tibi
Mbunge huyo anayejulikana kwa jina la Ahmed al-Tibi أحمد الطيبي alisema kupiga adhana ndani ya bunge hilo ni ishara ya kupinga muswada huo unaotaka kutotumika vipaza sauti wakati wa upigaji Adhana.

Al tibi wakati anapiga Adhana, wabunge wengi walisimama huku wakipiga kelele za kumtaka Spika amzuie kuendelea kufanya hivyo.

Hata hivyo Al-Tibi aliendelea mpaka kumaliza na kusoma dua baada ya Adhana na kwenda kukaa katika nafasi yake.

"Sheria hii inaonesha kukua kwa ufashisti ndani ya Israel na vitongoji vyake" alisema Tibi.

Pia alimshutumu Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kwamba yeye ndiye aliyesimamia muswada huo mpaka kufika Bungeni.
Mbunge Ahmed Al Tibi
"Wapalestina na Waislamu kote duniani wanapaswa kufanya kazi kuzuia azimio la Israel la kuzuia Adhana" alisema.

Ahmed al-Tibi ambaye amekuwa mbunge tangu mwaka 1999, mara kadhaa amekuwa akilishutumu bunge hilo kuwa ni la kibaguzi na lisilo na utu.

Al Tibi pia ni kiongozi wa chama cha  Arab Movement for Change (Ta'al).

Serikali ya Israel kupitia kamati ya sheria imepeleka bungeni muswada wa sheria utakapiga marufuku upigaji wa Adhana kwa kutumia vipaza sauti.