Saturday, 22 October 2016

WAISLAMU NCHINI ITALIA WATAKA RUHUSA YA KUTAMBULIWA MISIKITI YAO ZAIDI

Mamia ya waislamu nchini Italia jana walisali karibu na jengo la makumbusho la kikristo mjini Roma katika swala ya ijumaa baada ya kuzuiliwa na kufungwa kwa misikiti yao. 
Hali hiyo imefuatia baada ya misikiti mitano mjini Roma kufungwa na sehemu kadhaa walizozitenga maalumu kwa ajili ya kusalia kufungwa na mamlaka ya mji huo kwa madai haijapata usajili wa kisheria.

Msemaji wa taasisi ya Kiislamu ya Lazio Muslim Association, Francesco Terri alizitaka mamlaka zenye kuhusika zifanye utaratibu wa haraka wa kisheria kuruhusu na kutambua sehemu ambazao wamezitenga kwa ajili ya ibada zao.
Aidha walitoa wito kwa mamlaka husika kulinda haki
zao za kidini na kudai kupewa maeneo kisheria kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za ibada. 

Nchi ya Italia ina idadi ndogo ya Misikiti ambayo imesajiliwa kisheria ambayo haikidhi wingi wa waumini wanaosali.

Waislamu nchini Italia wanakadiriwa kufikia milioni 1.6 wanaosali katika misikiti inayotambuliwa rasmi. 

Uislamu ni dini ya pili kwa ukubwa nchini Italia baada ya ukatoliki, lakini haitambuliwi rasmi wakati dini ya uyahudi inatambuliwa rasmi japo wachache katika nchi hiyo.