Sunday, 23 October 2016

PICHA: JANET JACKSON NDANI YA BURQA NA MUMEWE JIJINI LONDON

Janet Jackson Jumatano wiki hii alijitokeza hadharani akiwa amevaa Burqa vazi la stara na mumewe Wissam Al Manna katika jiji la London nchini uingereza. 
Janet anaelezwa alisilimu tangu mwaka 2012 alipoolewa na Bilionea wa Qatar Wissam Al Manna mwenye umri wa miaka 41.
Janet anatarajiwa kujifungua karibuni na kupata mtoto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 50. 
Janet aliwahi kuolewa mara mbili huko nyuma kabla ya kuolewa na Wissam.
Hii ni mara yao ya kwanza kutokea hadhrani tangu vyombo vya habari viliporipoti Janet ana ujauzito.

Picha hizi zinawaonesha ni watu wenye furaha wakiwa jijini London katika maeneo ya Regent's Park kaskazini mwa jiji la London.
Wakizungukia maduka
Janet na Mumewe