Hafla hiyo ilihudhuriwa na watu wengi wakiwemo wageni kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania. Mgeni Rasmi alikuwa ni Sheikh Abdallah Jamzuri kutoka Lukozi.
Wengine waliohudhuria ni Sheikh Ahmad Issa, Sheikh Adam, Sheikh Omar Alfaj wa moshi, sheikh Mussa Nasib, Mwalimu halima Suluta na mwanafunzi wa Alhabib Omar Bin hafidh, Fatma Albeity.Dua maalum kwa ajili ya watoto iliongozwa na Alhaj Sheikh Yusuf Muhammad Kidago ambaye pia ndiye kiongozi wa zawia ya Ahbaabur Rasuul.
Pamoja na taratibu za dua pia watoto hao walionesha kwa kusoma masomo yao mbalimbali waliyojifunza katika madrasa zao.
Huu ni mwaka wa nane tangu kuanzishwa kwa utaratibu wa kuwaombea dua watoto na ni jambo ambalo kwa zama hizi ni muhimu mno kulingana na kuharibika kwa maadili.
Ahbaabur Rasuul inawaombea watoto wote kwa Mwenyezi Mungu makuzi yaliyo mema, yenye kheri na mafanikio ya duniani na Akhera.