Monday, 17 October 2016

JUMBA LA KUMBUKUMBU YA MAONESHO YA QURANI KUFUNGULIWA MAREKANI FEBRUARI 2017

Maonesho makubwa ya Quran yanatarajiwa kufunguliwa katika jumba la kumbukumbu la Smithsonian nchini Marekani
Maonesho hayo makubwa ya Quran yatakayofunguliwa kwa mara ya kwanza nchini Marekani, yameandaliwa chini ya ushirikiano wa usimamizi wa jumba la kumbukumbu la Smithsonian na shirika la hifadhi za kazi za utamaduni wa Kiislamu na Kituruki.

Maonesho hayo yatafunguliwa rasmi tarehe 20 Februari 2017 kwenye jumba la kumbukumbu la Smithsonian lililoko katika mji mkuu wa Washington nchini Marekani.

Miongoni mwa Quran zaidi ya 60 zitakazojumuishwa kwenye maonesho hayo ni zile zilizoandikwa kwa mkono kutoka ulimwengu wa Kiarabu, Uturuki, Iran na Afghanistan.