MUDIR wa Mahdi (Chuo) Shamsul Maarifa ya Tanga Sheikh Samir Sadiq amefiwa na Baba yake Mzazi aitwaye Sadiq Hemed Tunutu jijini Dar Es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Mzee sadick amefariki katika Hospital ya TMJ ya jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa tangu siku ya Jumanne akitokea katika mjini Tanga.
![]() |
| Mudir Sheikh Samir Sadiq |
Maiti ipo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na itasafirishwa leo kuelekea Tanga kwa ajili ya mazishi. Mazishi yanatarajiwa kuwa kesho katika makaburi ya Duga jijini Tanga.
Taarifa zaidi za mipango ya mazishi fuatilia hapa hapa katika Blogu yako ya Ahbaabur Rasuul.
Mwenyezi Mungu amsamehe makosa yake na alifanye kaburi lake kuwa moja ya Mabustani ya peponi.
