Monday, 31 October 2016

BABA WA DR ZAKIR NAIK AFARIKI DUNIANI, ASHINDWA KUHUDHURIA MAZISHI KWA KHOFU YA KUKAMATWA

Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un (إِنَّا للهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعونَ)  Sura Al-Baqara, aya 156.‎

MHUBIRI maarufu duniani Dr Zakir Naik amefiwa na baba yake aitwaye Abdulkarim Naik siku ya jumapili huko Mumbai nchini India.
Abdul karim Naik
Baba yake huyo alifariki akiwa na Miaka 87 na amezikwa jana na shughuli za mazishi zilifanyikia nyumbani kwake Rosery, mazgaon na kusaliwa maeneo ya Nariyal wadi qabrastan.

Taarifa zinasema Dr Zakir Naik hakuweza kuhudhuria katika mazishi ya baba yake kwa khofu ya kukamatwa na serikali ya India kwa shutuma kadhaa.

Serikali ya India inamuona Dr zakir kama mchochezi na mtu anayehimiza ugaidi duniani na kuleta vurugu katika jamii ya waislamu kutokana na mahubiri yake. 
Dr Zakir Naik
Hata hivyo aliwakilishwa na kaka yake Muhammad na mtoto wake Fariq na ndugu wengine katika msiba huo.

Kwa sasa Dr Zakir yupo nchini Malaysia na anatarajiwa kwenda kuhani muda wowote msiba wa baba yake nchini India. Dr Zakir ndiye mmiliki wa televisheni ya satalaiti ya Peace TV.

Baba yake alizaliwa mwaka 1928 huko Ratnagiri katika pwani ya Maharashtra.

Mwenyezi Mungu amsamehe makosa yake na alifanye kaburi lake kuwa moja ya Mabustani ya peponi.